Mechi za Azam FC vs Simba, Yanga kupigwa Chamazi
Mechi za Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga dhidi ya Azam FC zimepelekwa Azam Complex, Chamazi ambapo ndiyo uwanja wa nyumbani wa klabu ya Azam FC.

TFF imetangaza kwenye ratiba mpya kuwa michezo ya Simba na Yanga dhidi ya Azam FC, kuanzia sasa itachezwa katika uwanja wa Azam Complex tofauti na awali ambapo mechi hizo zilikuwa zinachezwa uwanja wa Taifa ambapo Shirikisho la Soka nchini (TFF) lilidai kuwa ni kutokana na ukubwa wa mechi.

Safari hii, Azam FC itaikaribisha Klabu ya Simba, Jumamosi hii ya septemba 9 mwaka huu mechi ya mzunguuko wa kwanza wa ligi kuu na baadae kuvaana na Yanga Jumamosi ya Tarehe 29 Desemba kunako dimba la Chamazi Complex .
Watch this
No comments