Bella wa Yamoto Band afunguka Ukweli kuhusu yeye kufunga ndoa kimya kimya

Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Enock Bella aliyekuwa member wa kundi la Yamoto Band amefunguka taarifa zinazodai amefunga ndoa.
Muimbaji huyo akizungumza na Dbash TV amesema si kweli kwamba amefunga ndoa kama inavyozungumzwa na picha kuonekana ila itakafika wakati atazungumza.
“Kwa sasa hivi nitadanganya siwezi kuzungumzia hilo suala, kuna wakati nitazungumzia tu ila kuna vitu fulani naviweka sawa. Hapana siwezi kusema nimefunga ndoa au sijafunga ndoa” amesema Enock Bella.
Hapo jana wasanii wenzake aliokuwa nao Yamoto Band, yaani Aslay, Beka Flavor na Maromboso walionekana kumpongeza Bella kupitia mitandao ya kijamii kwa kuashiria amefunga ndoa.

No comments

All rights are recieved.. Theme images by LonelySnailDesign. Powered by Blogger.