Wahamiaji haramu 74 wakamatwa Mtwara

Idara ya Uhamiaji imewakamata wahamiaji haramu 74 raia wa Ethiopia walioingia nchini kinyemela
. .

Aidha Wahamiaji 67 kati yao walikuwa wamejificha kwenye miti ya Mikoko katika Kisiwa cha Memberwa Msangamkuu huku wengine 7 wakikamatwa Wilayani Tandahimba.

Afisa uhamiaji Mkoani Mtwara Mratibu Mwandamizi wa Jeshi hilo James Mwanjotile amesema tukio hilo limetokea majira ya saa 12 jioni, baada ya kupata taarifa toka kwa raia wema, ambapo pia wamefanikiwa kumkamata mtanzania mmoja Bakari Said mkazi wa Tanga aliyewasaidia wahamiaji hao kuingia nchini kwa kutumia boti wakitokea Mombasa, na kwamba baada ya kupekuliwa, wahamiaji 16 walikutwa na hati za kusafiria, lakini hazina muhuri wa kuwaruhusu kuingia nchini. .

Aidha amewaonya watanzania wanaopenda kuwasaidia wahamiaji haramu kuingia nchini, kuacha vitendo hivyo kwa kuwa ni kinyume cha sheria na adhabu yake ni faini ya shilingimilioni 20 au kifungo cha miaka 2
0.

No comments

All rights are recieved.. Theme images by LonelySnailDesign. Powered by Blogger.