FUNZO:Zingatia mambo yafuatayo ili upate usingizi wa kutosha na wenye uhakika:
.
2. Epuka mazoezi muda mfupi kabla ya kulala Mazoezi ni muhimu lakini yanapaswa kupangiwa muda wake ambao hauingiliani na muda wa kulala. Ukifanya mazoezi joto la mwili linapanda na linachukua muda kupungua na kurudi katika hali kawaida. Inashauriwa kufanya mazoezi masaa 5 kabla ya kwenda kulala. .
3. Usitumie eneo la kulala kwa shughuli nyingine Chumba ambacho kimetengwa maalumu kwa ajili ya mapumziko hakipaswi kutumika kwa shughuli nyingine. Mfano kutumia chumba kama sehemu ya kusomea au kula chakula. Chumba cha kulala ni kwa matumizi mawili tu yaani kulala na kufanya tendo la ndoa.
.
4. Jiandae kisaikolojia Kila jambo tunalofanya linaanzia kwenye ubongo ambako shughuli zote za mwili huratibiwa. Jitahidi kuielekeza akili katika kulala. Wakati kulala sio wa kufikiri mambo yaliyotokea mchana au mambo mabaya yaliyotokea. .
5. Epuka kunywa pombe, kahawa na tumbaku kabla ya kulala Vinywaji na vilevi hivyo vina ‘caffeine’ ambayo huondoa usingizi. Vinywaji kama pombe na kahawa huamsha mwili na kuufanya mwili uchangamke na ukivitumia muda mfupi kabla ya kulala itakuchukua muda mrefu mpaka upate usingizi.
No comments