Injini ya Ndege yaharibikia angani, Watu 500 wanusurika kifo


Abiria 500 wamenusurika kifo baada ya injini moja ya ndege ya abiria ya shirika la Air France kuharibika ikiwa angani.
Ndege hiyo aina ya Airbus 380 (superjumbo) ilikuwa njiani kuelekea Los Angeles nchini Marekani ikitokea Paris, Ufaransa ikiwa na zaidi ya abiria 500.
Ndege hiyo iliamua kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Goose Bay, mashariki mwa Canada.
Ndege hiyo ikiwa imetua nchini Canada kwa dharula.
Abiria waliokuwemo ndani ya ndege hiyo wameeleza kuwa walianza kuona cheche zikitoka kwenye injini na ndipo walipoanza kutoa taarifa kwa wahusika.
Tulianza kuona cheche kwenye injini kitu ambacho sio cha kawaida kwani zilikuwa zinaongezeka kila muda ulivyokuwa unaenda huku ikitoa mlio mkubwa kitu ambacho kilizua taharuki ndani ya ndege.“amesema  Sarah Eamigh kwenye mahojiano yake na gazeti la New York Daily News.
Tayari shirika la Air France limethibitisha kutokea kwa hitilafu na hakuna mtu hata mmoja aliyejeruhiwa katika tukio hilo, huku wakieleza chanzo cha tatizo hilo kuwa ni kuharibika kwa feni za injini.
Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la AFP ndege hiyo ilikuwa na abiria 496 na wafanyakazi 24.

No comments

All rights are recieved.. Theme images by LonelySnailDesign. Powered by Blogger.