Mchekeshaji Mau ampa Shavu Jay Moe, amfananisha na kinyonga
Msanii wa Filamu Bongo, Mau Fundi amewachana wasanii wa zamani walioshindwa kubadilika kuendana na muziki sasa huko akimpongeza Jay Moe kwa kuweza kuendana na hali sasa.
Muigizaji huyo ameiambia E-Newz ya EATV kuwa muziki umebadilika na vijana wanakuja kwa kasi, watu hawataki tena uwaandikie verse nne/tano bali muziki wa sasa hivi ni ujanja na teknolojia imebadilika, hivo msanii anapawa kuwa mbunifu zaidi.
“Unaona hata Jay Moe kakubali hali ya hewa hii imebadilika, kikubwa hapo ni kuwa kinyonga, kwa hiyo wanamuziki wa kipindi hicho wanatakiwa wawe kinyonga,” amesema Jay Moe.
Mau amewataja wasanii walioshindwa kubadilika ni Bwana Misosi, Wagosi wa Kaya, Suma G, Chelea Man, Pig Black, Rapi na Zay B, huku akiongeza kuwa kuna wengine kibao.
No comments