Manchester United ni kiboko yao EPL

Ligi kuu nchini Uingereza imeendelea tena hii leo kwa michezo kadhaa kupigwa huko Old Traford, Manchester United imeng’ara mbele ya Crystal Palace baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 katika mchezo huo.
Waliyokuwa tishio katika ngome ya Palace ni mchezaji, J Mata ambaye alianza kufungua kikapu cha mabao dakika ya tatu ya mchezo, Fellaini akishinda mawili dakika ya 35 na 49 huku Romelu Lukaku akihitimisha idadi hiyo ya mabao dakika ya 86.
United iliyochini ya kocha raia wa Ureno, Jose Mario dos Santos Mourinho inaongoza Ligi hiyo kwa kuwa na jumla ya pointi 19 baada ya kushuka dimbani mara saba ilhali mpaka sasa Crystal Palace imefungwa jumla ya mabao 17 katika michezo 7 iliyoshuka dimbani huku ikiwa haina bao hata moja.
Katika michezo mingine Huddersfield imekubali kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya Tottenham.
Mchezaji nyota wa timu hiyo, Harry Kane ameendelea kutamba baada ya kutupia mawili katika ushindi huo huku B Davies akifunga moja na Sissoko akihitimisha la nne.
Na klabu ya Bournemouth imetoka sare ya bila kufungana dhidi ya Leicester  huku timu ya Stoke City imechomoza na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Southampton wafungaji wa City akiwa ni mchezaji M Diouf  na P Crouch wakati wageni wakipata bao la kufutia machozi kupitia kwa M Yoshida.
Wakati klabu ya West brom Albion ikitoka sare ya mabao  2-2  dhidi ya Watford, huku wagonga nyundo wa London timu ya West ham ikichomoza na ushindi mwembamba wa bao 1-0 mbele ya Swansea bao likifungwa na D Sakho dakika 90 ya mchezo.

No comments

All rights are recieved.. Theme images by LonelySnailDesign. Powered by Blogger.