"Nimechoshwa kusikia neno 'Watu wasiojulikana'-Waziri Mwigulu.

Neno watu wasiojulikana limekuwa maarufu sana tangu kipindi cha mauaji ya baadhi ya viongozi katika maeneo ya Kibiti. Lakini neno hilo lilizua gumzo kubwa baada ya kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na watu wasiojulikana ndio waliofanya tukio hilo na matukio mengine yaliyowahi kutokea.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema kuwa suala la watu wasiojulikana ni la muda tu kwani amechoka kusikia neno hilo.
Kauli hiyo Waziri Mwigulu Nchemba imekuja baada ya Azam two kumuhoji kuwa watu wanataka kujua watu wasiojulikana ni wakina nani hao, ndipo alipoweza kueleza jinsi anavyochukizwa uhalifu unaofanywa na watu hao(wasiojulikana).
“Me mwenyewe nachukia sana hilo neno watu wasiojulikana na kukimbilia kusiko julikana nilisema hata nilipokuwa kule Kibiti  kwamba nimechoka kusikia watu wasiojulikana wamekimbilia kusiko julikana nikawaambia nataka watu hawao wajulikane na wapelekwe kunako  julikana  kwa maana hiyo ni neno linalo maanisha wahalifu ambao hawakutia nguvuni katika kipindi hicho lakini,” alisema Waziri Nchemba.

“Nikwambie suala la wasiojulikana ni la muda tu watajulikana tu tutafumua hata unyasi tukigundua wamejificha kwenye unyasi huo lazima tutakomesha aina yoyote ya uhalifu.”

No comments

All rights are recieved.. Theme images by LonelySnailDesign. Powered by Blogger.