Mwanamke hata uwe mzuri vipi huwezi kuolewa Rwanda kama huna sifa hii

Inawezekana kila mtu ana vigezo vyake katika kutafuta mwanamke wa kuoa na hii inatokakana na aina ya familia, Utamaduni wa eneo au wakati mwingine hata nchi husika.
Sasa nchini Rwanda katika mkoa wa kusini wilaya ya Bugesera, Wanaume hawaangalii kigezo cha uzuri wala tabia bali kigezo chao kikubwa ni lazima mwanamke ajue kuendesha baiskeli na kama hajui basi atakaa na uzuri wake hadi azeekee nyumbani.
Wanaume katika mkoa huo ambao una tabu ya maji huoa wanawake wanaojua kuendesha baiskeli kwa kuamini kuwa watakuwa msaada mkubwa kwenye ndoa hii ni kutokana na umbali wanaotumia kuteka maji.
Hata hivyo tayari wanawake wa wilaya hiyo wameshajiwekea utamaduni wa kujifunza kuendesha baiskeli tangu wakiwa watoto ili kujiwekea nafasi nzuri ya kuolewa pindi umri wao utakapofikia.
Wilaya ya Bugesera ni moja ya wilaya ambazo zimezunguukwa na maziwa ila kutokana na uhaba wa miundo mbinu wanawake hulazimika kuyafuata maji safi umbali wa kilometa hadi 10 kila siku.
Ukiwa eneo hili ni ngumu kukuta mwanamke anashindwa kuendesha baiskeli, huu ni utamaduni wa watu wa mkoa wa kusini kwani wanaume wa huku wanaamini mwanamke akijua kuendesha baiskeli basi ataweza kumudu kuishi kwenye ndoa“,amesema Janvier Popote mwandishi wa habari wa gazeti la Rwanda Times na Izuba Rirashe kwenye mahojiano yake na Bongo5.
Hata hivyo ameongeza kuwa hata mwanamke akitoka eneo lingine au hata nchi nyingine na akawa anaweza kuendesha usafiri huo wa gharama ya chini basi kuolewa inakuwa ni rahisi zaidi.
Watu wengi hapa Bugesera hawaangalii sura wala maumbo pengine ni kwa vile wanawake wengi ni wazuri na tumezoea kuwaona wakiwa warembo siku zote, Wanaume wanahitaji mtu atakayeweza kuendesha baiskeli hicho ndio kigezo cha wananchi wa wilaya hii na kama mwanamke hajui kuendesha baiskeli basi atakaa kwa wazazi wake mpaka azeeke labda apate bwana ambaye sio mkazi wa wilaya hii.“amesema Janvier Popote.

No comments

All rights are recieved.. Theme images by LonelySnailDesign. Powered by Blogger.