Mwandishi aliyepotea miezi miwili kichwa na miguu yake vyapatikana ufukweni
Kichwa na miguu ya mwandishi wa habari wa Sweden, Kim Wall vimepatikana ufukweni, baada ya mwili wa mwandishi huyo kupotea miezi miwili iliyopita akiwa kwenye ziara ya kikazi na baharia raia wa Denmark.
Kim Wall
Kichwa na miguu ya Bi. Wall imeokotwa na waogeleaji katika fukwe za Koge mjini Copenhagen, Denmark ijumaa ya wiki hii vikiwa vimefungwa na mabegi .
Polisi mjini Copenhagen wamethibitisha kupatikana kwa kichwa na miguu ya mwandishi huyo wa habari ambapo wameeleza kuwa kwenye mabegi kulikuwa visu na vyuma vizito vilivyompelekea kuzama chini ya bahari.
Mkutano wa polisi na waandishi wa habari uliofanyika jana (Jumamosi) kuhusu tukio hilo kwa lugha ya Kidenishi.
Hata hivyo Bwana Peter Madsen (46) amekamatwa na polisi kwa mahojiano tangia tukio hilo lilipotiwe na vyombo vya habari nchini Sweden.
Polisi imesema kwenye mahojiano na mtuhumiwa huyo amekana kumuua huku akidai aliingia kwenye nchini kufanya uchunguzi kwa bahati mbaya akafa ndipo akachukua uamuzi wa kumtupa baharini.
Awali taarifa kutoka Associated Press zilieleza kuwa mwanadada huyo huenda alibondwa na vitu vizito akiwa kwenye manuari lakini tayari polisi wamekanusha taarifa hizo kwa kusema fuvu la kichwa cha Bi. Wall halikuwa na hitilafu wala dalili za kupigwa na kitu kizito.
Bi. Wall alipanda manuari hiyo ya Denmark akitokea Sweden akiwa na Baharia Madsen ambapo alikuwa akifanya habari za uchunguzi kama mwandishi wa habari.
Wall alikuwa ni Mwandishi wa Habari wa kujitegemea na amewahi kufanya kazi na magazeti makubwa duniani kama The New York Times, The Guardian na Foreign Policy
No comments