Nyashinski ataka malipo ya 20m kwenye interview, Wakenya wamvaa

Ni kweli Nyashinski ameanza kulewa umaarufu? Hiko ndio kitu kinachoonekana kwa msanii huyo kutoka kwa mashabiki na wadau wa muziki wa nchini Kenya.
Tuhuma hizo zimeibuka kupitia gazeti maarufu nchini Kenya baada ya msanii huyo kudaiwa kutaka kulipwa kiasi cha shilingi milioni moja za Kenya ambazo ni sawa na milioni 20 za Kitanzania katika kila interview atakayoalikwa.
“Alisema anataka tumlipe ndio aje kwenye show. Asipochunga ata-fade haraka. Nasikia amekuwa akiifanya hata studio fulani hivyo. Kwani yeye ni nani?,” limeandika gazeti hilo wakati wakimnukuu mmoja ya waaandishi ambao walikataliwa na Nyashinski kufanya mahojiano.
Nyashinski amedaiwa kuwa alikataa kufanya mahojiano hayo na kipindi kikubwa nchini humo cha runinga ambacho kinaruka kila siku za Ijumaa usiku.
Wakati huo huo Dbash TV imemtafuta mmoja ya waandishi kutoka nchini humo amethibitisha kuwa hiyo ndio tabia mpya ya msanii huyo na ameanza kuwavimbia mpaka wasanii wenzake kwa kuwakatalia kufanya nao kolabo.


Recommended videos for you








JIUNGE NA DBASH MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter  ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Dbash TV!

No comments

All rights are recieved.. Theme images by LonelySnailDesign. Powered by Blogger.